Migahawa ya KFC yakatazwa kuuza kuku waliotibiwa na Antibiotic

277
0
Share:

Kentucky Fried Chicken ni kampuni iliyopo maeneo ya Kentucky, Louisville huko nchini Marekani wakijihusisha na maswala ya upikaji wa nyama ya kuku na kuuza maeneo mbalimbali duniani wakiwa na takribani miaka 86 tangu mwaka 1952 katika uuzaji na usambazaji wa biadhaa zao katika maeneo mbalimbali.

Kampuni hiyo imeonywa kuchinja kuku waliotibiwa kwa madawa ya kuua sumu au Antibiotiki, huku mapendekezo hayo yakiwasilishwa na mashirika yanayowakilisha makundi 350000 nchini Marekani kufuatia kuibuka madawa hayo yanaathiri walaji wake.

Tayari KFC imeahidi kupunguza matumizi ya madawa hayo ya binadamu kwa kuku kuanzia mwaka Ujayo huku wanaharakati wakidai kuwa sera nchini Marekani zinaruhusu matumizi ya dozi ya binadamu kwa kuku jambo ambalo hupelekea walaji wa kuku hizo kutumia madawa hayo bila kukusudia.

Madawa hayo hutumika kwa ajili ya kukuzia kuku kwa haraka ili watimize vigezo vya uzani na hivyo faida kubwa katika muda mchache huku msemaji wa KFC akieleza kuwa anathamini athari iliyopo kwa wateja wao kabla ya kutoa vigezo vipya vya kuimarisha ubora wa kuku watakaochinjwa.

Wiki iliyopita maduka ya Mcdonald pamoja na Pizza Hut walipiga marufuku kununua kuku waliotibiwa kwa tiba zinazotumika kwa binadamu yaani Antibiotic.

Na Derick Highiness

Share:

Leave a reply