Mkazi Geita, Muhere Mwita anauza kiwanja chake ili akatibiwe nyonga nje ya nchi

405
0
Share:

Mkazi wa Geita, aliyefahamika kwa majina, Muhere Mwita ameamua kuuza kiwanja chake kilichopoeneo la Geita Mjini Nyankumbu  kwa bei ya Tsh. 3.5 Milioni.

Akizungumza kwa njia ya simu na MO BLOG iliyotaka kufahamu endapo fedha hizo ni kwa matibabu ya Hospitali ya hapa nchini ama nje ya Tanzania ambapo alieleza kuwa, kwa sasa ameshahuriwa na kaka yake akatibiwe nchini Kenya ili kunusuru mateso anayoyapata sasa.

“Nipo katika mateso makali sana. Nasumbuliwa na nyonga baada ya kupata ajali ya gari Mkoani Dodoma Oktoba 2016. Nilitibiwa kule na kisha Muhimbili lakini kwa sasa nimerejea nyumbani huku nikiendelea na kliniki Muhimbili. Naombeni wasamalia wema msaada wa haraka sana maana maumivu ni makali na sasa natafuta pesa nikatibiwe nchini Kenya kama nilivyoshahuriwa na ndugu” alieleza Mwita.

Hata hivyo, Mwita amesema kuwa, kama ataenda nchini Kenya  kupatiwa matibabu hayo, amepiga mahesabu ya haraharaka yanafikia kiasi cha zaidi ya fedha za Kitanzania Milioni 3. Hivyo ameamua kuliuza kiwanja chake hicho kiasi hicho hicho cha Milioni 3.5  ili aende haraka kupata matibabu.

“Kwa yoyote atakae kuwa tayari anaweza kuwasiliana na mimi kwa mawasiliano yangu ya Simu namba 0742530600. Ili nipate  msaada wa haraka unahitajika” ameeleza Mwita.

Bwana Mwita aliueleza mtandao huu wa MO Blog kuwa, tokea kufanyiwa operesheni Muhimbili ya Nyonga yake iliyovunjikavunjika amekuwa akiishi kwa mateso makubwa ya maumivu makali huku mpaka sasa akiwa amwshatumia gharama nyingi za matibabu zilizofikia kiasi cha Tsh. 4 Milioni.

Kwa wanaohitaji kiwanja hicho kwa haraka zaidi ambapo amesema kina Upana wa  25 na Urefu wa 38, kipo katika eneo zuri  kwa anayehitaji anaweza kwenda kukiona.

MO BLOG inamtakia msaada wa haraka Bwana Mwita hii ni pamoja na kwa mtu yeyote mwenye uwezo anaweza kuwasiliana naye ama kufika Geita kwa msaada zaidi.

Picha ya nyonga yenye kuvunjika

Muhere Mwita anayehitaji msaada wa haraka akiwa katika  baiskeli ya wagonjwa

Share:

Leave a reply