Mkutano wa wadau wa elimu wafungwa, Serikali yaahidi kufanyia kazi maazimio

200
0
Share:

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandishi, Musa Iyombe amesema Serikali itahakikisha inatekeleza maazimio yote yaliyopitishwa kwenye Mkutano wa pamoja wa mwaka wa wadau wa Elimu uliofanyika kwa siku nne Mjini Dodoma.

Eng. Iyombe ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa wadau wa Elimu wenye lengo la kujadili changamoto, mafanikio ya Elimu na kuona namna gani kama wadau wanaweza kutafuta njia ya pamoja ya kuboresha Mfumo wa utoaji wa Elimu Tanzania.

“Nimepokea maazimio yote ya Mkutano huu na nitayawasilisha panopo husika kwa ajili ya Utekelezaji lakini pia niwapongeze kwa kazi kubwa mliofanya, kuanzia wataalamu kutoka Serikalini, sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa Elimu, hakika mmefanya kazi kubwa na kupitia Mkutano huu tutaona mabadiliko makubwa katika Sekta hii muhimu,” alisema Iyombe.

Akitoa salamu za Wizara Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Sylivia Temu amesema Kikao kimekuwa na tija kwa kuwa pamoja na mambo mengine kimejadili masuala yanayotokana na utafiti wa elimu na kwamba matokeo ya tafiti yaliyo onesha changamoto yatafanyiwa kazi kwa pamoja kati ya serikali, wadau wa maendeleo wakiwepo mashirika yasiyo ya serikali.

Wadau wa Elimu nchini wamekutana mkoani Dodoma katika ukumbi wa Hazina kwa muda wa
siku tano ikiwa ni juma la elimu Tanzania na kuajadili kwa pamoja chanagamoto na mikakati yakuboresha elimu ili kumtoa mtoto wa kitanzania katika elimu duni.

Na Nteghejwa Hosseah- TAMISEMI

Share:

Leave a reply