Mkuu wa Chuo ajiuzulu kwa kukosa ushirikiano kutoka kwa walimu

816
0
Share:

Mkuu wa Chuo cha Krinshnagara Women’s College nchini India, Dkt. Manabi Bandopadhyay ametoa kali ya kufunga mwaka baada ya kuandika barua kwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya nchini humo akitaka kujiuzulu nafasi hiyo.

Bandopadhyaya amesema kwamba ushirikiano hafifu kutoka kwa walimu na wanafunzi umesababisha yeye kuamua kujiuzulu wadhifa wake ili kupisha mtu mwingine mwenye maono tofauti achukue nafasi yake.

Amesema kwamba tabia ya walimu na wanafunzi katika chuo hicho cha wasichana pekee na kwamba maamuzi yake yalichukuliwa vibaya kutokana na jinsia yake.

Bandopadhyay 50, alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa chuo hicho cha elimu nchini India kuanzia Juni 2015 na alisimamia shughuli za utawala za kila siku kwa takribani mwaka mmoja na nusu.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na vyombo vya habari, Bandopadhyay aliwatupia lawama jamii ya India kwa kumtesa kimwili na kiakili kutokana na jinsia yake baada ya kuwa mkuu wa chuo hicho maarufu nchini India.

Lakini alisisitiza kwamba pamoja na changamoto zote hizo alifanikiwa kupata shahada yake ya uzamivu na baadaye kuwa Profesa.

Share:

Leave a reply