Mnangagwa aahidi uchaguzi kuwa wa haki na huru

152
0
Share:

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameahidi kwamba nchi yake itaendesha uchaguzi huru na wa haki utakaofanyika kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

Mnangagwa aliyasema hayo katika Mkutano wa Uchumi Duniani (World Economic Forum – WEF) unaofanyika mjini Davos, Uswizi na kueleza kuwa hivi karibuni wataanza maandalizi ya uchaguzi huo.

“Mwezi ujao tutaanza maandalizi ya uchaguzi, kwhiyo ninaamini ucahguzi hautakuwa Julai, inaweza kuwa mapema kabla ya Julai,” alisema Mnangagwa.

Aidha Mnangagwa alisema atakubali matokeo hata kama wapinzani watakuwa wameshinda.

Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza kwa Zimbabwe tangu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe kujiuzulu mwezi Novemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Emmerson Mnangagwa ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais.

 

Share:

Leave a reply