MODEWJIBLOG “Team” inawatakia heri ya Pasaka wasomaji wetu

208
0
Share:

Leo ni siku ya Pasaka ambapo Wakristo Duniani kote wanasheherekea siku hii muhimu ikiwemo kulitukuza jina la Bwana Yesu Kristo maana yeye alifanyika kuwa mwanakondoo kwa ajili ya ukombozi wake ili wanaadamu tuokolewe kutoka katika dhambi kama nukuu za vitabu takatifu (1 Korintho 5 : 7).

Hivyo uongozi mzima wa mtandao pendwa wa Modewjiblog unapenda kuwatakia heri ya Pasaka na pia unatoa rai kwa Jamii nzima kuhakikisha wanazingatia suala la amani na usalama wa mali zao hasa majumbani na sehemu watakazokuwa katika kusheherekea siku hii ya leo.

Tujiepushe na matumizi ya vileo kupita kiasi, tusiendeshe vyombo vya moto kwa kasi, pia familia zenye watoto wadogo wasiwaruhusu watoto wao waende kutembea bila waangalizi ilikuepuka matatizo yanayokuwa yanajitokeza mara kwa mara juu ya wimbi la kupotea watoto.

Endelea kusoma mtandao wako bora wa Modewjiblog kwa habari kemkem za kila siku popote pale zinapotokea tunakupatia hapa hapa..

 

Share:

Leave a reply