Mohamed Salah ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika 2017

314
0
Share:

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2017.

Salah ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda kura wenzake wawili ambao ni Sadio Mane anayekipiga Liverpool na timu ya Taifa ya Senegal na Pierre-Emerick Aubameyang anayechezea klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Gabon.

Katika kura zilizopigwa na wanachama wa CAF, Salah amepata kura 625, Mane 507 na Aubameyang kura 311.

 

Orodha kamili ya washindi wa tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika 2017.

Mchezaji Bora Afrika 2017 – Mohamed Salah (Liverpool/Misri)

Mshindi wa pili – Sadio Mane (Liverpool/Senegal)

Mshindi wa tatu – Pierre Emerick Aubameyang (Dortmund/Gabon)

Mchezaji Bora wa Mwanamke wa Mwaka – Assisat Oshoola (Nigeria)

Timu Bora ya Taifa ya Mwaka – Misri

Mchezaji Bora wa Mwaka Anayechipukia – Patson Daka (Zambia)

Kocha Bora wa Mwaka – Hector Cuper (Misri)

Kalbu Bora ya Mwaka – Wydad Athletic Club (Morocco)

Kiongozi Bora wa Soka wa Mwaka – Ahmed Yahya

Timu Bora ya Wanawake ya Mwaka – Bayana Bayana (Afrika Kusini)

CAF Legends Award: Ibrahim Sunday (Ghana)

Platinum award to Ghana president Nana Akufo-Addo & Liberia president-elect George Weah

Share:

Leave a reply