Moto wateketeza bweni la Shule ya Sekondari Katunguru mkoani Mwanza

473
0
Share:

Moto mkubwa umezuka na kuteketeza bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari Katunguru iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza huku chanzo chake kikiwa hakifahamiki.

Hayo yamethibitishwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Baraka Ezekiel Msimba ambapo amesema moto huo umetekeza vitu vyote vilivyokuwa ndani ya bweni hilo huku wanafunzi  takribani 5 wakinusurika kifo. 

Kufuatia ajali hiyo mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo huku akiahidi kuchangia akiahidi kuchangia magodoro 50 mifuko 50 ya saruji Mkuu wa mkoa ameagiza kuanza ujenzi wa mabweni hayo mara moja.

Nao wanafunzi wameeleza kwa majonzi juu ya kuteketea kwa vifaa vyao vya kujisomea na kwamba wamesikitishwa zaidi na ajali hiyo ya moto.  

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Sengerema amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii licha ya kukumbwa na ajali hiyo.

Na Veronica Martine

Share:

Leave a reply