Moto waua watu watatu Nairobi, Kenya

216
0
Share:

Mamia ya watu katika mtaa wa Kijiji, mjini Nairobi Kenya, wamekesha nje usiku wa kuamkia leo baada ya kukosa mahali pa kulala kutokana na nyumba zao kuteketezwa na moto mkubwa.

Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika, ulizuka na kuenea kwenye mtaa huo, majira ya saa mbili usiku  jana Januari 28, 2018. 

Magari ya zima moto hayakufanikiwa mapema kuuzima moto huo kwa kushindwa kufika eneo la tukio kutokana na ufinyu wa barabara na kulazimika kuuzima kwa mbali hadi yalipoishiwa na maji.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Kukabiliana na Majanga nchini Kenya, Pius Masai aliliambia gazeti la Nation kwamba walilazimika kuomba msaada wa kuzima moto huo. Baadae magari ya kuzima moto ya baraza la jiji yalifika na baadae moto huo kuzimwa.

Wakazi wa mtaa huo waliviambia vyombo vya habari kuwa moto huo umeteketeza mali, biashara na wengine makazi.

Share:

Leave a reply