Mourinho amwakikishia nafasi Schweinsteiger

478
0
Share:

Maisha ya kiungo mkongwe wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger ndani ya klabu hiyo yanaonekana kuendelea kuwepo kwa muda zaidi baada ya kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho kuweka wazi mipango ya kumtumia katika michezo inayofata ya timu hiyo. 

Mourinho amesema kwasasa atamtumia Schweinsteiger katika Ligi ya Vilabu Ulaya kutokana na idadi ya wachezaji alionao na idadi ya michezo iliyopo mbele yao hivyo ili waweze kucheza bila kuathiri mfumo wao wa uchezaji ni vyema kuwapa nafasi na wachezaji wengine ambapo na mkongwe huyo atakuwepo..

“Ndiyo, atabakia na atakuwa kwenye listi ya Ligi ya Vilabu Ulaya. Kuna nafasi ambazo ziliachwa na Memphis Depay and Morgan Schneiderlin [wameondoka] na hatuna wachezaji wengi katika eneo la kiungo,” alisema Mourinho.

Aidha Mourinho alizungumza kuhusu kiwango cha Schweinsteiger katika mchezo wa Wigan, “Dakika tisini kwake zilikuwa ni ngumu. Kuanzia dakika ya 65, 70 alikuwa na wakati mgumu. Lakini ilikuwa muhimu kwa mwili wake. Ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa hata ambapo anakuwa hachezaji anabaki kuwa yule yule. Kwa mashindano na dakika nyingi tulizonazo ana nafasi.”

Schweinsteiger amepata nafasi ya kwanza kucheza kwa dakika 90 katika kikosi cha Man United kinachonolewa na Mourinho katika mchezo kombe la FA wakati Man United ikicheza na Wigan, mchezo huo ulimalizika kwa United kushinda goli 4-0 huku Schweinsteiger akifunga goli moja na kutoa pasi ya goli moja.

Share:

Leave a reply