Mourinho awapa makavu Wenger na Van Gaal, akataa Rooney kucheza nafasi ya kiungo

182
0
Share:

Limekuwa jambo la kufurahisha kwa kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho kuwa akirushiana maneno na kocha mwenzake wa Arsenal, Arsene Wenger tangu alipokuwa akiifundisha Chelsea na sasa ambo hilo limeanza kujirudia akiwa na Man United.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari, Mourinho alionekana kuzungumza maneno ambayo yalionekana wazi kumlenga Wenger pamoja na kocha aliyepita kuinoa Manchester United, Louis Van Gaal.

“Mameneja wengine wameshinda kombe miaka 10 iliyopita na wengine hawajaweza kabisa. Mara ya mwisho mimi nimeshinda kombe mwaka uliopita, kwahiyo kama nina vitu vingi vya kurekebisha basi linganisha na wengine,

“Ukweli ni kuwa hilo jambo sio muhimu kwangu, ninacheza dhidi yangu mwenyewe, nina mambo ya kuboresha kwangu sio kwa ajili ya wengine ila mimi na hiyo ndiyo kawaida yangu, siwezi kufanya kazi bila mafanikio,” alisema Mourinho.

Aidha kocha huyo alimzungumzia Giggs na kusema kuwa ” Sio wajibu wangu kuwa Giggs hayupo klabuni, kazi ambayo Ryan alikuwa akihitaji Manchester United ni kuwa meneja,

“Hilo sio wajibu wangu, wamiliki na Mr. Woodward walinitaka mimi na ni muda ambao Ryan alitaka kuwa meneja, hata mimi nilichagua kuwa kocha miaka iliyopita lakini wengi wetu tunaanza kwa kuwa makocha wasaidizi,” alisema kocha huyo.

Kuhusu nafasi ya Rooney katika kikosi chake, Mourinho alisema “Jambo moja ambalo siwezi kulibadili ni kuhusu kubadili nafasi yake ya kufunga magoli, anaweza asiwe mshambuliaji, lakini kwangu hawezi kuwa namba 6, atacheza ndani ya mita 50 kutoka goli la adui,

“Wachezaji wengi wanauwezo wa kutoa pasi lakini kazi ngumu ni kufunga magoli, anaweza kuwa namba 9 au namba 10 au namba 9.5 lakini sio namba 6 au 8,” aliongeza Mourinho.

Share:

Leave a reply