Msaidizi wa Wayne Rooney ahukumiwa kifungo cha miezi 32 gerezani

740
0
Share:

Mahakama ya Chester Crown nchini Uingereza imemkuta na hatia aliyewahi msaidizi wa nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney kwa kosa la kujaribu kumwibia bosi wake huyo hivyo kumhukumu kifungo cha gerezani kwa miezi 32 (miaka miwili na miezi nane).

Mtu huyo ambaye anafahamika kwa jina la Robert McNamara anadaiwa alijaribu kuingia katika nyumba ya Rooney wakati mchezaji huyo akiwa katika mchezo maalum uliozikuanisha Manchester United na Everton, mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Akizungumza kuhusu tukio hilo mahakamani, mke wa Rooney, Coleen alisema tukio hilo liliwafanya wawe na hofu kuhusu usalama wao na hasa pindi ambapo watoto wao wanapokuwa wakicheza katika bustani hivyo kuwafanya kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kuimarisha usalama.

McNamara alionekana kujaribu kuingia katika nyumba ya Rooney kupitia za kamera za CCTV ambazo zimefunga katika nyumba kisha kukamatwa baada ya siku sita tangu afanye tukio hilo na kufunguliwa kesi mahakamani ambapo amepewa adhabu hiyo.

Share:

Leave a reply