Mshindi wa Mr. Tanzania kunyakua gari aina ya Noah na Tsh. Milioni 10, kufanyika Desemba 16

689
0
Share:

Shirikisho la ujenzi wa mwili Tanzania (Tanzania Bodybuilding Federation-TBBF) kwa ushirikiano na Pilipili Entertainment Limited,  wanatarajia kufanya shindano kubwa na la la aina yake hapa nchini juu ya Ujenzi wa Mwili yaani ‘MR. TANZANIA’ kwa mwaka 2017.

Wakizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Septemba 19,2017, Jijini Dar es Salaam, viongozi wa TBBF, wamebainisha kuwa tayari uitikio mkubwa kwa wa watu mbalimbali wamejitokeza na sasa wapo kwenye mazoezi ya kujifua kwa aajili ya shindano hilo.

Akizungumza namna walivyoandaa tukio hilo, Katibu Mkuu wa TBBF,Bw. Francis Mapungilo amesema kuwa, uitikio umekuwa mkubwa nan tayari washiriki wapo kwenye kambi zao ‘Gym’ wakiendelea kujifua kujiandaa na shindano hilo.

“Kwanza kabisa leo tungependa kuwajulisha kuwa, TBBF tutashirikiana na kituo cha Azam tv kuonyesha matukio yote ya shindano hili ambalo ni halisi (reality show) kupitia  Azam tv 2),  Mchakto uliopo ni wa majaji kuwaengua wale ambao hawajafikia zile sifa tajwa katika kambi maalum itakayoanza Desemba 12, mwaka huu, ambapoo pia kutafuatiwa na semina ya mashindano yenyewe ambapo washiriki watakaopita kwenye mchujo huo watajengewa uwezo na mafunzo mbalimbali” alieleza Francis Mapungilo.

Aidha, Francis Mapungilo ameongeza kuwa, katika shindano hilo, mshindi wa kwanza anatarajia kujinyakulia gari aina ya Noah pamoja na kitita cha Tsh. Milioni 10 taslimu huku  mshindi wa pili akitarajiwa kuondoka na donge nono la Tsh Milioni 5 na wa tatu ataibuka na kitita cha Tsh. Milioni 2.5.

Mbali na zawadi hizo pia zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wengine ikiwemo Style Icon,  Mr. Handsome na Mr. Photogenic  huku pia kila ‘Gym’ itakayotoa mshindi itaibuka na zawadi ya kitita cha Tsh. Milioni 5.

Hata hivyo, wamebainisha kuwa, taratibu zote ikiwemo za upatikanaji wa tiketi  kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo wanatarajia kubandika kwenye mtandao wao wa: www.tzbbf.org pamoja na mitandao mingine mbalimbali.

Na Andrew Chale-MO BLOG

Mwenyekiti wa mashindano hayo, Bw. Nilesh Batty akizungumza katika tukio hilo 

Logo ya shindano hilo

Katibu Mkuu wa TBBF,Bw. Francis Mapungilo akizungumza katika tukio hilo mapema leo Septemba 19,2017.  Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Nemes Chiwalala nan kulia ni Mkurugenzi wa ufundi, Bw. Fike Wilson.

 Mwenyekiti wa chama TBBF, Nemes Chiwalala  akizungumza katika tukio hilo. Kushoto kwake ni Mzee Chillo mshahuri wa kampuni ya Pilipili Entertainment. Wengine Kulia ni Katibu wa TBBF, Francis Mapungilo, akifuatiwa na Mkurugenzi wa ufundi, Bw. Fike Wilson. Akizungumza wakati wa tukio hilo.

Share:

Leave a reply