Msuva, Anthony waing’arisha Yanga ikiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi Esperance

217
0
Share:

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga imeibuka kidedea katika mchezo wa kwanza wa mchujo kutafuta nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Sagrada Esperance ya Angola.

Mashujaa wa Yanga katika mchezo huo alikuwa ni Simon Msuva ambaye aliifungia Yanga goli la kuongoza dk. 71 na Matheo Anthony aliyefunga goli la pili katika dakika za majeruhi.

Baada ya ushindi huo, mchezo wa marudiano unataraji kuchezwa Mei, 17 nchini Angola.

Share:

Leave a reply