Mtanzania afungua duka la nguo za Kitanzania nchini Marekani

951
0
Share:
Mtanzania Lilian Danieli mwenye kampuni yake ya NASHONA amefungua duka la nguo za Kitanzania Goldsboro jimbo la North Carolina nchini Marekani. Uzinduzi wa duka hilo ambalo lipo Center Street katikati ya mji huo wa Goldsboro ulifanyika siku Jumamosi March 25, 2017.
Awali wakati wa uzinduzi huo aliwashukuru watanzania na watu mbalimbali wakiwemo wageni wanaofika kulitembelea duka hilo kwani anajisikia furaha kuitangaza Tanzania katika Taifa kubwa  kama hilo la Marekani.
“Karibuni watu wote. Duka hili limesheheni nguo za kitanzania na ni halisi kutoka matirio halisi ya nyumbani. Anuani ya kufika dukani ni 119 Center Street, Goldsboro, NC ama watu wenye kutaka oda wanaweza kuasiliana nami moja kwa moja simu ya dukani ni 918 947 1273. Alielleza Mtanzania huyo Lilian Danieli.
 
Aidha, Mtanzania huyo ameweka wazi kuwa miongoni mwa nguo hizo ni vitenge mbalimbali toka Tanzania ikiwa asilimia 90 ameshona yeye mwenyewe na baadhi ya vingine kuja toka Tanzania.
 
Baadhi ya wateja waliokuwepo dukani hapo siku ya uzinduzi wa duka hilo Jumamosi March 25, 2017 Goldsboro, North Carolina nchini Marekani.
Lilian Daniel Kulia akikinja moja ya nguo zilizo nunuliwa na mmoja ya wateja wake siku ya uzinduzi wa duka lake la nguo za kiTanzania lililozinduliwa siku ya Jumamosi March 25, 2017.
Kushoto ni Serena Danieli akisaidiana na dada yake Imani Danieli katika kuhakikisha mahesabu ya duka yanaenda sawa.
Lilian Danieli akiwa na mmoja ya wateja wake akiwaonyesha nguo zake na kuwapa maelekezo.
Mmoja ya wateja akilipia kitu alichonunua.
Mahitaji ya manunuzi yakiendelea.
Picha zote na Vijimambo Blog na Kwanza Production, Marekani.
Share:

Leave a reply