Mtanzania ashiriki filamu Marekani, acheza nafasi ya Kevin Durant (Video)

624
1
Share:

Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kung’ara. Safari hii mtoto wa watanzania wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.

Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi. 

Juu, katika clip mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake.

Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony. 
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake. 
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.
Pamoja na kucheza filamu hiyo pia Evan amefanya audition nyingi kwahiyo Mungu akipenda ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu zaidi. 
Unaweza kuona clips za hiyo movie kupitia links hizi za Youtube. 

Share:

1 comment

Leave a reply