MTN BUSHFIRE 2017 – kufanyika Mei 26-28 mwaka huu nchini Swaziland

485
0
Share:

Tamasha kubwa la muziki la MTN Bushfire, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini  Swaziland kuanzia Mwezi Mei 26 – 28. 2017, ambapo likitarajia kukusanya watu mbalimbali kutoka Duniani kote ambao watajumuika pamoka kufurahia na kucheza muziki mzuri kutoka kwa wasanii na bendi za pande zote za dunia.

MTN Bushfire ni miogoni mwa tamasha kubwa la muziki na lenye mvuto zaidi linalifanyika Afrika. Aidha miongoni mwa listi ya wasanii watakaotumbuza jukwaani kwa mwaka huu ni pamoja na 80 Script (Swaziland), Baloji (congo), Ben day & the concrete lions (Afrika Kusini), Bombino, Chico Antonio (Msumbiji),Dj Bob (Afrika Kusini), Faada Freddy (Senegali/Ufaransa), Femi Koya, Flame Boy universe (Swaziland), Goodluck (Afrika Kusini),  Gren Seme.

Wengine ni Kwesta,  Matthew Mole, Michael Canfield,Msaki, Petite Noir ,The Jaigermeister brass Cartel ft. Reason,Rootsword, Sands, Seba Kaapstad, Siyinqaba,The Kiffness, Hugh Masekela, Jah Prayzah, Jeremy Loops, Jojo Abot, Kids n Cats na  Mkongwe wa Kwaito kutoka Afrika Kusini  Tkzee.

Tamasha la MTN Bushfire ni linadhaminiwa na MTN huku likiwa ni  miongoni mwa matamasha 7 makubwa Barani Afrika ambayo umvutia mtu kiuhalisia kwa mujibu wa CNN huku pia likitajw akuwa ni miongoni mwa matamasha 10 bora ya Kimataifa kipindi cha Summer.

 

Na Andrew Chale-MO BLOG

Moja ya maonyesho ya tamasha hilo yaliyopita

Share:

Leave a reply