Mtoto wa Hoyce Temu, Ruby Sikutwa asheherekea siku ya kuzaliwa na watoto wa Uhuru mchanganyiko

413
0
Share:

Mtoto wa mrembo wa taji la Miss Tanzania 1999 na mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten, Hoyce Temu, Ruby Sikutwa tarehe 29 Mei, 2016 ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya kutumiza miaka 6 kwa kula chakula cha mchana na watoto wa shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko pamoja na marafiki zake katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam.

Hoyce Temu ambaye ndie mama mzazi wa Ruby ameandaa sherehe hiyo na kuwaalika watoto kutoka Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko ambao wengi wao wana Ulemavu wa ngozi, viungo, wasioona na wasiosikia ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo kwa jamii lakini pia kumjenga mtoto wake Ruby katika makuzi yake kuwa karibu na watu wa aina mbalimbali bila kubagua.

Ruby Sikutwa Birthday Party

Birthday Girl Ruby Sikutwa akiimba wimbo maalum uliokuwa ukiongozwa na Mzee Njenje aliyekuwa akitumbuiza na bendi yake katika hoteli hiyo.

Ruby Sikutwa birthday cake

Birthday Girl Ruby akimlisha cake rafiki yake wa karibu.

Ruby Sikutwa na Mama wakubwa

Mama wakubwa wa Birthday Girl Ruby Sikutwa wakipozi kwa Ukodak.

Ruby Sikutwa handing over gift to friends

Birthday Girl, Ruby Sikutwa akigawa zawadi kama asante kwa ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika nae kwenye chakula cha mchana katika hafla ya kusheherekea kutimiza miaka 6.

Ruby Sikutwa Birthday Lunch

Watoto wa shule ya msingi Uhuru Mchangayiko na marafiki wa Ruby Sikutwa wakipata chakula cha mchana.

Hoyce Temu chatting with Uhuru mchanganyiko student

Mrembo wa taji la Miss Tanzania 1999 na mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na watoto wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko baada ya chakula cha mchana.

Hoyce Temu hand over a gift to her daughter

Hoyce Temu akimkabidhi zawadi mtoto wake Ruby Sikutwa.

Ruby Sikutwa receiving a gift from Grandmother

Ruby Sikutwa akipokea zawadi kutoka kwa bibi yake.

Ruby Sikutwa receiving a gift from Aunty Sara

Birthday girl Ruby Sikutwa akipokea zawadi kutoka kwa Mama yake mkubwa Sara.

Madam Sophy Mbeyela

Madam Sophy Mbeyela ambaye ni rafiki wa karibu na Hoyce Temu akimkabidhi zawadi birthday girl Ruby.

Ruby Sikutwa na mama mkubwa

Birthday Girl Ruby Sikutwa na mahaba tele kutoka kwa Mama Mkubwa.

Shamim Mwasha na Hoyce Temu

#Ahsante kwa Kuja: Hoyce Temu akimkabidhi zawadi rafiki yake Blogger maarufu, Shamim Mwasha wa 8020 Fashions.

Monica Joseph a.k.a Monifinance

Hoyce Temu akitoa zawadi ya asante kwa kuja kwa rafiki yake Mtaalamu wa masuala ya fedha nchini, Monica Joseph a.k.a Monfinance.

Usia Nkhoma Ledama

Hoyce Temu akimshukuru rafiki yake Usia Nkhoma Ledama kujumuika katika chakula cha mchana kusheherekea miaka 6 ya kuzaliwa kwa binti yake Ruby Sikutwa.

Hoyce Temu zawadi kwa Hellen

Hoyce Temu akiendelea na zoezi la kushukuru marafiki waliojumuika kwenye chakula cha mchana.

Hoyce Temu

Imelda Mtema

Hoyce Temu akimshukuru Mwandishi wa Global Publishers, Imelda Mtema kushiriki kwenye chakula hicho cha mchana maalum kwa binti yake Ruby Sikutwa.

Ruby Sikutwa group photo

Birthday girl Ruby Sikutwa katika picha ya pamoja na watoto wa Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko na marafiki zake wa karibu.

Group Photo

Birthday girl Ruby Sikutwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa walioshiriki nae katika chakula cha mchana.

Ruby Sikutwa na Emirates Air hostess

Birthday girl, Ruby Sikutwa akipongezwa na wafanyakazi wa Shirika la ndege la Emirates kwa kutimiza miaka 6 ya kuzaliwa kwake.

Sara Temu

Mama yake mkubwa na Ruby, Sara Temu akibadilishana mawazo na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyioko.

Shamim Mwasha

Kutoka kushoto ni Hoyce Temu, Shamim Mwasha wa 8020 Fashions na Zoe Glorious.

 

Share:

Leave a reply