Mtu mmoja afariki kwa kunywa pombe ya kienyeji Sengerema

396
0
Share:

Mtu mmoja amekutwa akiwa amefariki dunia katika mtaa wa Geita Road wilayani Sengerema mkoani Mwanza akidaiwa kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi.     

Wakizungumza na MO Blog kwa masikitiko makubwa ndugu wa marehemu wamedai kuwa baba huyo alitoka nyumbani mapema jana majira ya saa nne asubuhi na hakuweza kuonekana mpaka majira ya usiku na ndipo walipoanza kumtafuta bila mafanikio.

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la Polisi katika eneo hilo Seni Mboje amesema kuwa baba huyo  amemkuta maeneo ya mabanzini usiku wakuamkia leo mnamo saa saba usiku akiwa amelewa pombe na saa kumi na moja alfajiri baba huyo ndipo alipofikwa na mauti hayo.

Hata hivyo wananchi wa mtaa huo wametoa ushauri wao kwa watu wanaofanya bishara ya pombe za kienyeji wawe makini kwa watu wenye umri mkubwa ikiwemo wazee kuwauzia pombe hiyo.

Aidha mwenyekiti wa eneo hilo amewaasa wananchi kuwa makini na pia watoe taarifa mapema pale mtu anapoingia eneo lolote bila taarifa.

Na Emmanuel Twimanye

Share:

Leave a reply