Mtulia alitaka tena jimbo la Kinondoni, atangaza kuchukua fomu

186
0
Share:

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo La Kinondoni kupitia chama cha Wananchi (CUF) Maulid Mtulia, ambaye hivi karibuni alijiuzulu ubunge wa jimbo hilo baada ya kujiunga na Chama tawala CCM, kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli, leo Desemba 19, 2017 ameibuka na kutangaza kwamba atachukua fomu ya kuomba ridhaa CCM ili agombee tena jimbo hilo.

Kupitia taarifa yake iliyosambaa mchana wa leo Jumanne ya Disemba 19, 2017 kwenye mitandao ya kijamii, ambayo yeye mwenye Mtulia aliuthibitishia mtandao huu kuwa ni taarifa yake, inaeleza kuwa, iwapo CCM itaridhia kumruhusu kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio wa Januari 13 mwakani, atagombea.

“Kwanza, nawasalimu wote na hasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Pili, nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF.Tatu, nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu,” amesema na kuongeza.

“Hivyo basi, nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni.Mimi mtumishi wenu.”

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply