Mugabe afuta ziara ya kuchukua tuzo nchini Ghana

293
0
Share:

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefuta ziara yake ya kwenda nchini Ghana kupokea tuzo ya Millennium Lifetime Achievement award, kwa kuliongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika kupata uhuru wake mwaka 1980.

Rais wa Ghana John Mahama alitarajiwa kumpa Mugabe tuzo hiyo, katika warsha inayotarajiwa kufanyika mji mkuu wa Ghana Accra.

Mugabe mwenye umri wa miaka 92, ameingoza Zimbawe tangu ipate uhuru na ameapa kusalia madarakani hadi kifo na kukataa wito wa kumtaka ang’atuke.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa safari hiyo, lakini mtandao mmoja nchini Ghana unawanukuu wanadiplomasia nchini Zimbabwe wakisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana masuala ya kisiasa nchini Zimbabwe.

Mabango makubwa yalikuwa yamewekwa mjini Accra kumkaribisha Rais Mugabe huku hotuba yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply