Mugabe amtuhumu Rais Mnangagwa kutumia jeshi

339
0
Share:

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametuhumu njia iliyotumika kumng’oa madarakani kwa madai kwamba alikuwa tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa, Emerson Mnangwagwa ili kuleta mabadiliko ya uongozi ya uhalali.

Mugabe amedai kuwa, Rais Mnangwagwa alitumia nguvu ya jeshi kumlazimisha kutoka madarakani, hatua aliyoikemea kuwa haikuwa ya uhalali.

Mugabe ameonyesha kutokuamini kitendo hicho kufanywa na Mnangwagwa kwa kuwa alimuamini, vile vile yeye ndiyo aliyemuingiza serikalini pamoja na kumtoa gerezani alipotaka kunyongwa.

Hata hivyo amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais Mnangwagwa ili waweze linda katiba ya nchi hiyo.

Share:

Leave a reply