Muhammad Ali Jr. aikimbia familia yake

263
0
Share:

Muhammad Ali Jr ambaye ni mtoto wa mwana masumbwi, Muhammad Ali, ameamua kuiacha familia yake na kuhamia kwenye nyumba ya urithi iliyoachwa na baba yake aliyefariki Juni, 3 baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Familia ya Ali, akiwemo mjane Lonnie Ali pamoja na watoto wake tisa walikutana Juni 28 mwaka huu kwa ajili ya kugawana mali za baba yao huyo, ambapo waligawana mali sawasawa.

Lonnie yeye alikabidhiwa jumba la kifahari la mume wake Ali, huku Ali Jr akikabidhiwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 80.

Katika hali iliyoonekana ni ya kushangaza, Ali Jr alimpatia mke wake, Shaakera, dola za kimarekani 75 tu kwa ajili ya kununua chochote kitakachompendeza, lakini pia aliwanunulia wanae viatu vipya huku yeye akiondoka kwa ajili ya kutafuta mahali patakapofaa kwa biashara.

Aidha ilisemekana kuwa, Ali Jr amedhamiria kuanzisha biashara kubwa pamoja na kusaidia jamii hasa watu wasiojiweza.

Ali Jr pamoja na Shaakera walizaa pamoja watoto wawili, Ameera, 8, na Shakera mwenye umri wa miaka 7.

Muhammad Ali ambaye ni mzaliwa wa Lousville, Kentucky huko nchini Marekani alifariki dunia kutokana ugonjwa wa Kupooza ulioanza miaka ya nyuma na ameacha watoto tisa ambapo watoto 7 ni wa kike na 2 ndio wa kiume.

Na Derick Highiness

Share:

Leave a reply