Muuaji wa watu 39 katika klabu ya usiku Istanbul ajulikana

963
0
Share:

Serikali ya Uturuki imethibitisha kumtambua mmoja kati ya watu wawili ambao walishiriki kuwaua watu 39 katika klabu moja ya usiku iliyopo mji mkuu wa nchi hiyo, Istanbul usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2017.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu amesema muhusika ametambulika lakini kwa sasa bado hajatoa maelezo zaidi kuhusu yeye na jina lake bado hawajawa tayari kulitaja hadharani licha ya Polisi kutoa picha ya mtu huyo.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu kikundi cha kigaidi cha ISIS kudai kuwa kimehusika na shambulio hilo na kuwa wanamgambo waliohusika na shambulio hilo ni mashujaa kutokana na jinsi walivyoweza kuua watu wengi.

Katika tukio hilo wauaji wawili waliokuwa na silaha walimwua Polisi na mtu mmoja kisha kuingia ndani ya klabu ya usiku ya Reina na kuanza kupiga risasi ambazo zilisababisha vifo vya watu 39 ambao walikuwa ndani ya ukumbi huo.

Baadhi ya watu wanaendelea kushikiliwa na Polisi kwa kudaiwa kuhusika na tukio ambapo kati yao watano wanahisiwa kuwa wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha Islamic State (IS).

Share:

Leave a reply