Mvua yasababisha maafa Tabora, yaua watano

495
0
Share:

Watu watano wakazi wa wilaya ya Igunga, Tabora wamefariki duniani katika matukio mawili tofauti kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema hayo wakati wa mkutano  na waandishi wa habari.

Alisema kuwa katika tukio la kwanza mnamo tarehe 11 mwezi huu, watu wanne wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba waliokuwa wakiishi kufuatia mvua zilizonyesha kwa kipindi cha siku mbili.

Kamanda Mtafungwa alisema walifariki kwa kuangukiwa na ukuta wanatoka kijiji cha Igogo kata ya Nanga kuwa ni Kagwa Makenza (80) ambaye pia ni mmiliki wa nyumba iliyosababisha maafa hayo, wengine ni Sande Dule (6), Butonda Shija(3) na Mbula Dule mwenye miezi miwili.

Alisema watoto wote watatu walifariki dunia wakati wakipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Katika tukio la pili, Kamanda Mtafungwa alisema katika kijiji cha Bulyang’ombe kata ya Nanga mtoto Zenga Tano (5) alifariki dunia baada ya kupigwa na randi mnamo tarehe 10 mwezi huu wakati amelala na wazazi wake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alitoa pole kwa familia za waliopatwa maafa na kuwashauri wakazi wa Igunga kufuata utalaamu wa ujenzi wakati wa ujenzi wa nyumba zao ili kuepuka maafa zaidi.

Alisema kuwa ushauri huo ni pamoja na ujenzi katika sehemu ya miinuko kwa ajili ya kujikinga na maafa zaidi.

Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

Share:

Leave a reply