Mvua yaua watu tisa Dar

114
0
Share:

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema watu tisa wamepoteza maisha katika nyakati tofauti, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa.

“Mnano tarehe 14 Aprili 2018 majira ya saa tatu usiku huko maeneo ya Segerea mtaa wa mji mwema watu wawili ambao ni [email protected] Mama Elias (30) na Adulrazak Ally (4) wamefariki baada ya kuangukiwa na uzio wa ukuta wakiwa wamelala ndani ya nyumba. Ukuta huo wa uzio wa nyumba uliangukia nyumba ya vyumba vitano inayokaliwa na wapangaji,” amesema SACP Mambosasa na kuongeza.

“Aidha katika tukio hilo watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa hospitali ya amana kwa matibabu. Na miili ya marehemu ilipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi. Pia mnamo tarehe 15 Aprili 2018 majira ya saa saa nne usiku huko maeneo ya Goba Salasala nyumba ya chumba kimoja ilianguka na kusabisha kifo cha mtu mmoja aitwaye Mikidadi Hija (44).”

Amesema, katika tukio lingine, mnamo Aprili 15, 2018 maeneo ya Kigogo, Mwanaidi Seif (24) aliangukiwa na ukuta wa nyumba akiwa ndani na kufariki dunia, vile vile maeneo ya Temeke Sadick Ally (36) aliteleza na kutumbukia katika daraja la mto Kizinga lililokuwa limejaa maji na kusababisha kifo na kwamba Jitihada za kuutafuta mwili wa marehemu bado zinandelea.

“Mnamo Tarehe 16 Aprili 2018 huko maeno ya Mbagala misheni mtu mmoja Nasri Ally Haji (9) Mwanafunzi wa shule ya msingi Bokorani amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba akiwa amelala.Vile vile mnamo tarehe 15 Aprili 2018 huko Kinyerezi kwenye bonge la mto kinyerezi mtu mmoja jinsia ya kiume ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 35 alikutwa amekufa kutokana na kusombwa na maji,” amesema.

SACP Mambosasa ameongeza kuwa “Pia mtu mmoja jinsi ya kiume ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 35 alikutwa amekufa huko Kawe, Mbezi beach A, baada ya kusombwa na maji. Ambapo mwili huo umehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia mnamo tarehe 16 Aprili 2018 huko Kawe, salasala Amina Said (28) amefariki baada ya kangukiwa na ukuta wa nyumba akiwa amelala nyumbani kwake.”

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply