Mwalimu Mkuu wa Sekondari ajinyonga hadi kufa

1097
0
Share:

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Tumuli wilaya ya Iramba mkoani hapa, Richard Neligwa Makala (58), amefariki dunia baada ya kujinyonga.

Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa,ACP Debora Magiligimba alisema tukio hilo limetokea Februari, 26 mwaka huu saa moja asubuhi huko katika kijiji cha Tumuli tarafa ya Kinyangiri.

Alisema mwalimu huyo alitumia kamba aliyoitengeza yeye mwenyewe kwa vipande vya vyiandarua na kisha kuifunga juu ya mti.

“Baada ya kuifunga juu ya mti,alijifunga shingoni na kisha kujitupa na kuning’inia kwa lengo la kukatisha maisha yake. Mti huo upo  umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake,” alifafanua Magiligimba.

Kamanda huyo alisema kuwa hadi sasa chanzo cha kujinyonga kwa mwalimu mkuu huyo,bado hakijajulika.Juhudi za kubaini chanzo hicho,zinaendelea.

Alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari katika hospitali ya Nduguti na umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Na Nathaniel Limu, Singida

Share:

Leave a reply