Mwanawake masikini akuta dola za kimarekani 15 milioni kwenye akaunti yake, amwandikia Waziri Mkuu

485
0
Share:

Uttar Pradesh ambaye anakaa mji wa Sheetal Yadav alipatwa na mshangao na mshtuko baada ya kutoka kwenye ATM yake wiki mbili zilizopita na kukuta dola za kimarekani 15 milioni.

Mshangao wake uliwashtua wateja wengine baada ya kuanza kumuuliza mtu wa pembeni kama amesoma vizuri karatasi yake ya muamala ambayo ilionyesha kiasi hicho cha pesa.

Baadaye mwanamke huyo alilazimika kwenda ATM kadhaa kucheki salio kwenye akaunti akitegemea kupata majibu tofauti lakini salio lilikuwa ni lile lile.

Mwanamke huyo msamaria mwema ambaye ana mshahara wa dola 74 tu kwa mwezi alilazimika kwenda benki ilikupata ufafanuzi wa salio la kwenye akaunti yake.

Baada ya kufika benki aliambiwa kwamba arudi baadaye kwakuwa meneja hakuwepo lakini baada ya meneja kurudi alikataa kufanya chochote juu ya akaunti hiyo ya mwanamke huyo masikini.

Bi Yadav pamoja na mumewe Ziledar Singh waliamua kumwandikia barua Waziri Mkuu wa India ilikuweza kupata ufafanuzi juu ya jambo hilo la kushangazaa kwenye akaunti yake lakini mpaka sasa bado hajawapata majibu rasmi kutoka kwa ofisi ya Waziri Mkuu.

Share:

Leave a reply