Mwenyekiti wa TLP, Mrema awataka watanzania kutomgombanisha Rais Magufuli na Miimili ya nchi

269
0
Share:

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Dk. Augustine Lyatonga Mrema  ameibuka nan kuzungumza na vyombo vya habari mambo mbalimbali ikiwemo lile la kuwataka Watanzania kuacha kumtupia manung’uniko Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli huku pia akimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kupuuza ushahuri wa aliyewahi kuwa Mkuu wa jeshi hilo, Omary Mahita.

Akizungumza katika tukio hilo, Mh. Mrema amebainisha kuwa,  kwa sasa Tanzania hali ni shwari hivyo watanzania wanatakiwa kuwa na imani na Serikali iliyopo madarakani na kuacha kumgombanisha Rais na miimili mingine ya nchi ikiwemo Bunge na Mahakama.

“Hii miimili inajitegemea. Rais hana muda wa kuendesha hiyo miimili na anafanya kaz zake vizuri hivyo tuache masuala ya kumuhusisha Rais kwani  kumuonea. Kwenye miimili kuna watu wazuri na kuna watu wasio wazuri. Kama tunatoa hukumu basi tutoe kwa hao  ila sio Rais” alieleza Mh. Mrema.

Mrema amebainisha kuwa kwa sasa IGP Sirro hasikubali kupokea ushahuri wa  IGP mstaafu, Omary Mahita kwani wakati wa utawala wake hakufanya vizuri na hata kumbambikia kesi mbili za uongo.

“Namtaka IGP Sirro aachane na ushahuri wa Mahita, kwani aliwatesa watu na hata kuwabambikizia kesi. Mimi alinifungulia kesi mbili ikiwemo ile ya rushwa na ya kumtukana Rais Mkapa ambazo zote zilikuwa ni za uongo.Niliposikia Mahita anasema anataka kutoa ushahuri kwa IGP Sirro ndio maaana nimeibuka na kumuambia aachane na huo ushahuri utamwaribia ni bora atafute kwa watu wengine nikiwemo mimi nitaweza kumsaidia kwni nina uzoefu mkubwa katika masuala ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii” alieleza Mrema.

Na Andrew Chale, MO BLOG

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Dk. Augustine Lyatonga Mrema  akizungumza katika mkutano huo leo Septemba 20,2017

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Dk. Augustine Lyatonga Mrema akizungumza katika mkutano huo na vyombo vya habari mapema leo Jijini Dar e Salaam,Septemba 20,2017.

Share:

Leave a reply