Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI-ELIMU akagua kambi ya UMISSETA 2017

684
0
Share:

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Bw. Tixon Nzunda ameipongeza Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania ( UMISSETA) kwa maandalizi mazuri iliyoyafanya kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo kufanyika pamoja na muda mfupi iliyopewa.

Akizungumza wakati wa kukagua kambi ya Michezo ya Watoto wanaoshiriki katika Michezo ya UMISSETA kwa mwaka 2017 katika Chuo cha Ualimu Butimba Bw. Nzunda ameitaka Kamati ya Maaandalizi kufanya kazi kama timu kwa kuwa kushindwa kwa mmoja miongoni mwa wanatimu ni kushindwa kwa wote kwasababu hakuna anayeweza kufanya kazi peke yake na kufanikiwa kwakuwa wanategemeana.

Bw. Nzunda aliiagiza Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanawalinda watoto kwa kuhakikisha wanarudi salama mashuleni kwao.

“ Nidhamu ya kuwalinda watoto ianzie ndani ya sekretarieti ya maandalizi ili kuhakikisha watoto wanarudi salama mashuleni. Alisisitiza Bw. Nzunda

Aidha alitaka kila mkoa unaoshiriki katika mashindano kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri na kurudi na ushindi . Na wakati huo huo aliitaka Kamati ya Maandalizi kuhakikisha inafanya vizuri ili iweze kuwa Sekretarieti ya maandalizi ya kudumu ingawa alisema hatasita kuifuta iwapo Sekretarieti hiyo haitafanya vizuri katika majukumu yake.

Mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania( UMISSETA) kwa mwaka 2017 yanafanyika kitaifa Mkoani Mwanza na yanazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu  tarehe 08 Juni, 2017 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI( ELIMU) Bw. Tixon Nzunda akikagua sehemu ya kupikia chakula cha Wanafunzi wanaoshiriki katika mashindano ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Tanzania( UMISSETA) katika kambi ya mashindano hayo iliyopo katika    Chuo cha Ualimu Butimba kabla ya uzinduzi wa mashindano hayo unaofanyika tarehe 08 Juni, 2017.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI-ELIMU Bw. Tixon Nzunda akiwa na wajumbe wa Sekretarieti ya Maandalizi ya Michezo ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania( UMISSETA) katika kambi ya Michezo hiyo iliyopo katika Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza kabla ya kuzinduliwa kwa mashindano hayo.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI(ELIMU) Bw. Tixon Nzunda akizungumza na Sekretarieti ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mashindano ya Shule ya Shule za Sekondari Tanzania( UMISSETA)yanayofanyika jijini  Mwanza yanayozinduliwa rasmi tarehe 08 Juni, 2017 hadi 15 Juni, 2017. Kulia kwa Bw. Nzunda ni Kaimu Mkurugenzi anayeshughulikia Elimu kutoka TAMISEMI Bw. Maulid Ahmed na Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Butimba Bw. Apolinary Ndomba.

Share:

Leave a reply