Naibu Waziri Juliana Shonza aanza na wasanii

622
0
Share:

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, ametangaza mikakati yake ya kazi na kuahidi kuwashawishi wasanii nchini kuvaa mavazi yenye staha ili kuuenzi utamaduni.

Shonza ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa leo Oktoba 9, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema wasanii wengi hawavai mavazi yenye heshima mbele jamii.

“Changamoto kubwa ni kwenye mavazi, ningependa kuwaasa vijana wenzangu kwamba tuenzi utamaduni wetu, na niwaombe wasanii ambao kidogo imekuwa shida kwenye mavazi waenzi utamaduni wetu,” amesema.

Aidha, Shonza ameahidi kupandisha hadhi ya lugha ya Kiswahili ili izidi kutambulika kimataifa na kuwaingizia kipato watanzania.

“Suala la utamaduni ni pana, ukizungumzia utamaduni unazungumzia lugha yetu ya Kiswahili, nitahakikisha lugha inakuwa chanzo cha kuwaingizia vijana kipato na inakuwa kwa kuiongezea hadhi.Nitahakikisha nasiamia ilani ya ccm inayotuelekeza kuhakikisha habari zinapatikana kwa haraka na usahihi zaidi,” amesema.

Share:

Leave a reply