Naibu Waziri Mpina aongoza wakazi wa Mchikichini, Dar kufanya usafi

562
0
Share:

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhanga Mpina jumamosi ya Julai, 1 ameungana na wakazi wa Dar es Salaam ambao wanaishi katika kata ya Mchikichini iliyopo Manispaa kufanya usafi.

Naibu Waziri Mpina ameshiriki shughuli hiyo ikiwa ni sehemu utekeleza wa agizo la Rais John Magufuli la kila jumamosi wananchi kwa pamoja washirikiane kufanya usafi ili maeneo yao yawe safi jambo ambalo litsaidia kupungua kwa magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.

Akizungumza baada ya kumaliza kufanya usafi, Naibu Waziri Mpina aliwataka watendaji wa serikali katika maeneo yote kuhakikisha wananchi wanafanya usafi na kwa wote ambao watakuwa wanagoma kushiriki kufanya usafi wapeleke taarifa ngazi za juu ili wachukuliwe hatua.

“Tangu Rais Magufuli alipotoa agizo mmeona tumepiga harua kubwa ya maeneo yetu mengi kuwa masafi tofauti na ilivyokuwa awali, nawaagiza maafisa mazingira muhakikishe watu wanafanya usafi sio kila jambo mnalileta ngazi za juu hata nyie mnaweza kuwashughulikia sisi tuleteeni wale ambao wanaonekana ni wagumu,” alisema Mpina.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajenjere ambao ndiyo wanaohusika kukusanya taka katika eneo la kata ya Mchikichini, Ilala, Mathew Andrew amesema wananchi wanatakiwa kubadilika kwa kutumia taka kama njia ya kujiingia kipato.

“Taka ni mali na masoko yapo waziwazi hakuna sababu ya mwananchi kutupa zile taka, wananchi wanatakiwa wajue kuwa taka ni pesa na sisi (Kajenjere Trading Company) tumekuwa tukitoa elimu ili wanaanchi wajue jinsi wanavyoweza kupata pesa na zinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali na soko lake hapa hapa,” amesema Andrew.

Share:

Leave a reply