Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla afanya ziara kwenye Zahanati za Segerea, Tabata ‘A’ na kituo cha Afya Mnyamani Dar

194
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya,  Dk. Kigwangalla  afanya ziara kwenye Zahanati za Segerea, Tabata ‘A’ na kituo cha Afya Mnyamani

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Zahanati na Kituo cha Afya ndani ya Jimbo la Segerea kwa kile kilichoelezwa kusikiliza kero za Wananchi waliokuwa wakilalamikia huduma mbovu zilizokuwa zikitolewa na watumishi wa sehemu hizo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla aliongozana na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh.  Bi. Bona Kalua pamoja na watendaji wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala. Akiwa katika Zahanati ya Segerea, Dk. Kigwangalla aliweza kukagua kituo hicho  maeneo mbalimbali hata hivyo alipongeza kituo hicho

kwa miundombinu yake pamoja na hali ya utendaji wa kazi aliyoikuta hapo hata hivyo aliwataka kuhakikisha wanajenga chumba cha Upasuaji mdogo ambacho kitasaidia kutatua matatizo madogomadogo kwa wagonjwa watakaofikishwa hapo.

Dk. Kigwangalla amewapa miezi sita wasimamizi wa Zahanati hiyo kuhakikisha kuwa wanakamilisha chumba cha upasuaji mdogo ilikupunguza msongamano wa wagonjwa wa matatizo ya upasuaji ule mdogo ambao wengi wao wamekuwa wakirundikana katika Hospitali za Amana na Muhimbili wakati vituo hivyo vingekuwa na majengo hayo vingeweza kutatua tatizo hilo.

Kwa upande wa  Zahanati ya Tabata ‘A’,  Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla alitoa maagizo hayo hayo ya kuhakikisha nao wanakamilisha jengo la upasuaji kwa wagonjwa huku akimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Zahanati hiyo inapata eneo la kuongeza majengo yao ya Hospitali.

“Msongamano wa wagonjwa Hospitali ya Amana tunaweza kupunguza tu endapo changamoto kubwa na  ukosefu wa Maabara, vifaa vya kutosha pamoja na uwepo wa chumba cha upasuaji. Hivyo naagiza kwenye Zahanati hizi zote kuhakikisha zinajenga Vyumba hivyo vya Upasuaji haraka na ndani ya miezi sita nitarejea kukagua tena kama mumeweza kutimiza maagizo yangu ama la” alisema  Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo kwa Madaktari na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Kwa upande wake, Dk. Rumishael Mwanga ambaye ni Mganga Mkuu wa Zahanati ya Segerea alieleza kwamba amekua akikabiliana na changamoto ya chumba cha upasuaji hivyo kwa maagizo hayo watayafanyia kazi ndani ya miezi hiyo Sita kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

“Wanapokuja wagonjwa wenye uhitaji wa operation kubwa hua tuna waandikia waende hospitali ya Amana kutokana na ukosefu wa chumba cha upasuaji” alisema Dk. Mwanga.

Aidha katika tukio la kutembelea kituo cha Afya cha Mnyamani, Dk. Kigwangalla  aliagiza mara moja uongozi wa Kituo hicho kuhakikisha wanaongeza vitanda vya kutosha vya wagonjwa, pamoja na kupunguza watumishi waliozidi  na kuwapeleka kwenye vituo vilivyo pungukiwa watumishi wa kada hiyo.

Aidha, Dk. Kigwangalla aliutaka uongozi wa Kituo hicho kuhakikisha wanajenga chumba cha upasuaji  huku akiagiza kuhakikisha wanapata fursa ya kupanua eneo hilo la Kituo cha Afya ilikuweza kuwa na majengo mengi.

Na Laudanus Majani.

DSC_4594Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha kumbukumbu cha Wageni katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ilala. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Bi. Sophia Mjema  na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bi. Bona Kalua.

Dk. Kigwangalla alimtembelea Mkuu wa Wilaya huyo muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara yake kwenye Vituo vya Afya na Zahanati ndani ya Jimbo la Segerea.

DSC_4602

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala (DAS) Bwana  Edward Mpogolo wakitafakari jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa ziara katika Wilaya hiyo ya Ilala.

DSC_4604

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Segerea, Bona Kalua.

DSC_4609.Mganga Mkuu wa Zahanati ya Segerea, Dk.Rumishael Mwanga akimkaribisha  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kuwasili kwenye ziara hiyoDSC_4614

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa .Mganga Mkuu wa Zahanati ya Segerea, Dk.Rumishael Mwanga

DSC_4617 DSC_4621

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya kina kutoka kwa nesi anayeshughulikia wanawake wanaojifungua.

DSC_4652

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea maoni kutoka kwa wananchi na wagonjwa (Hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo

DSC_4655

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akimpa maelekezo mmoja wa wa Wanawake waliofika kwenye Zahanati hiyo ya Segerea kwa ajili ya kuhudumiwa

DSC_4662

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo ya kujengwa kwa chumba cha upasuaji kwenye Zahanati hiyo ya Segerea.

DSC_4664

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika Zahanati ya Tabata ‘A’ wakati wa ziara hiyo mapema leo Agosti 9.2016.

DSC_4671

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akisikilzia taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bwana. Msongela Palela

DSC_4684

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Ilala, Bwana Msongela Palela. 

DSC_4688 DSC_4693 DSC_4698

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kuhakikisha Mkurugenzi anapaata hati miliki ya eneo la kiwanja ambacho mmiliki wake awali aliahidi kutoa kiwanja hicho kwa ajili ya kupanua majengo ya Zahanati hiyo.

DSC_4711 DSC_4713Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuhakikisha wanalipa fidia wananchi ilikupata eneo la kuongeza majengo ya kituo cha Afya Mnyamani.

Share:

Leave a reply