Naibu Waziri wa Afya Dk. Kingwangalla amtembelea Mzee aliyebuni nembo ya Taifa Muhimbili

573
0
Share:

Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kingwangalla ameweza kumtembelea Mzee Francis Maige Ngosha ambaye amelazwa kwenye chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo awali alipelekwa hapo kwa uchunguzi wa afya na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana.

Mzee Maige ni mmoja w aliyebuni Nembo ya Taifa (Bibi na Bwana) ambapo hivi karibuni alilipotiwa na vyombo vya habari kuwa yupo katika hali hali ya kimaisha na kiafya.

(Picha na Catherine Sungura-WAMJW)

Naibu Waziri Dkt.Kingwangalla akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt.Mfinanga(kulia) mara baada ya kumjulia hali Mzee aliyebuni nembo ya Taifa Mzee Francis Maige kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Hospitali hiyo,kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Profesa Laurence Maseru

Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura Renatus Tarimo(kushoto)  akimueleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto jinsi walivyompokea na kumuhudumia kwenye kitengo chao na hali ilivyo hadi sasa,Dkt. Tarimo amesema hali ya Mzee maige inaendelea vizuri na wameshamfanyia uchunguzi wa awali na wanaendelea na uchunguzi zaidi

Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kingwangalla akiongea na Mzee Maige ambaye amelazwa kwenye chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo awali alihamishiwa hapo kwa uchunguzi wa afya na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana.

Share:

Leave a reply