“Naomba Agosti 7 msikutane kimwili na wenza wenu”- Raila Odinga

999
0
Share:

Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya Umoja wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amewataka wananchi nchini humo kutokutana kimwili na wenza wao Agosti, 7.

Odinga ameyasema hayo wakati akihutubia katika eneo la Homa Bay ambapo alisema wananchi wanatakiwa kujiandaa kwa uchaguzi ambao utafanyika Agosti, 8 na hivyo ni vyema siku hiyo wasikutane na wenza wao ili wajiandae kwa uchaguzi.

Katika kusisitiza hilo amewataka hata ambao wapo kwenye ndoa kufata ushauri wake na akiwataka wanawake kuwanyima waume zao unyumba hata kama wakitaka kufanya nao mapenzi.

“Tunakwenda kwenye vita tunahitaji kuwa na nguvu ya kutosha kabla hatujaingia kwenye vita Agosti 8, hakuna mtu kati yetu anatakiwa kufanya mapenzi usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi,

“Wanawake wote wanapaswa kuwanyima unyumba haki yao kwa usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi,” alisema Odinga wakati akiwahutubia wananchi na kuongeza.

“Tukifanya hivyo tutaweza kuamka mapema, tutapiga kura na kubakiwa tukiwa vizuri mpaka siku matokeo yanatangazwa.”

Share:

Leave a reply