Nassor Idrissa Mwenyekiti mpya Azam FC arithi mikoba ya Alhaji Said Mohamed

424
0
Share:

Aliyekuwa  Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa timu hiyo  ya Azam FC akirithi mikoba ya Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo, ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Idrissa.

Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29.2016.

Aliyekuwa  Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa akimkabidhi jezi ya timu hiyo, beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast baada ya kusaini Mkataba wa kujiunga (Pich ya Maktaba)

azam

Aliyekuwa  Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa (wa pili kutoka kulia kwenye picha wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda)

Share:

Leave a reply