Ndugu wa familia moja wakamatwa na Polisi kwa kupanga kufanya shambulizi

283
0
Share:

Kutokana na matukio ya mashambulizi kuzidi kushamiri katika maeneo mbalimbali duniani, Polisi nchini Ubelgiji imewatia mikononi watu wawili wa familia moja kwa kukisiwa kupanga kufanya shambulizi.

Taarifa kutoka Ubelgiji zinaeleza kuwa watu hao hao ambao ni mtu na mdogo wake waliofahamika kwa majina ya Nourredine na Hamza walikamatwa na Polisi baada ya kufanyika msako katika mji wa Liege.

Baada ya kukamatwa walifikishwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha baadae ndiugu mmmoja kuruhusiwa kutoka na mwingine akibaki kituoni.

Vyombo mbalimbali vya habari nchini Ubelgiji vimeripoti kuwa Nourredine amekuwa akijihusisha na vitendo vya uharifu na alikuwa akiwasaidia Wabelgiji kusafiri kwenda Syria kupambana katika vita.

Kwa siku za karibuni, polisi wa Ubelgiji wamekuwa wakifanya doria kubwa katika mji wa Liege na Bergen kutokana na maeneo hayo kukisiwa kuwa kumepangwa kufanyika mashambulizi.

Share:

Leave a reply