NEC Zanzibar kukutana katika kikao maalum cha Kamati Jumamosi hii ya Aprili 23

223
0
Share:

TAARIFA RASMI KUHUSIANA NA

KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR

 KWA VYOMBO VYA HABARI.

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanziba, kesho (Aprili 23, 2016) inatarajia kukutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari Jabu imesema kikao hicho kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, iliyopo mtaa wa Kisiwandui, Mjini Unguja.

Taarifa imesema kikao hicho kawaida cha siku moja, pamoja na mambo mengine kitapokea na kujadili taarifa kadhaa kutoka Idara na Vitengo mbali mbali vya Chama hicho, ikiwemo taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar, kabla na baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar.

Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, kilichofanyika  April 20, mwaka huu, chini ya M/kiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, kwa ajili ya kuandaa ajenda za kikao hicho.

Taarifa  imesema kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) ya Katiba ya CCM, Toleo la mwaka 2012 na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Imetolewa na:

Sgd.

(Waride B. Jabu),

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,

Idara ya Itikadi na Uenezi – CCM,

ZANZIBAR.

22/04/2016.

Share:

Leave a reply