NECTA yaboresha mfumo wa mawasiliano kuwabaini wanaotumia vyeti feki

2161
0
Share:

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi  kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa  kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine. 

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua  ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti  ambavyo sio vyao. 

Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au  taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine  kuwasiliana nao kupitia barua pepe [email protected] au simu namba +255  742 484 955. 

Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia  muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia  Jumatatu hadi Ijumaa. 

Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane  nao kupitia barua pepe [email protected] au simu namba 0658 116 644 kwa  saa za kazi. 

Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu  wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa  watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake. 

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO

Share:

Leave a reply