News Alert: Sudani Kusini yaingizwa rasmi nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

286
0
Share:

Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha, Tanzania Marais wanaoshiriki mkutano huo wameipitisha rasmi nchi ya Sudan Kusini kuwa mwanachama rasmi wa nchi za Jumuiya hiyo na kufanya kufikia nchi sita zinazounda Jumuiya ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na Sudani Kusini iliyoingizwa rasmi leo Machi 2.2016.

Wakuu wa nchi mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki na wajumbe wao wapo katika mkutano huo ambao pia umepitisha mambo mbalimbali ikiwemo hati ya kusafiria ya kielektroniki.

EA

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mkutano huo. Katikati ni  Rais wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli ambaye amekabidhiwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo ambapo atashikiria nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.

Share:

Leave a reply