Ney wa Mitego atangaza kupokea maoni ya Wapo Remix

1507
0
Share:

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ amesema kuwa sasa anpokea maoni kutoka wa watu mbalimbali ambao wanakero zinazowakera katika jamii wampe ili aimbe katika remix ya nyimbo ya Wapo.

Ney wa Mitego ameyasema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na kusema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kupokeaushauri kutoka kwa Rais Magufuli na Waziri Mwakyembe.

Aidha alimshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono juhudi ambazo anaonesha kuwasaidia wasanii wa tasnia mbalimbali nchini na kuwa amepokea ushauri kutoka hata kwa Rais ambao ataufanyia kazi katika Wapo remix ambayo hajaitaja itatoka lini.

“Namshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga mkono pia naahidi kufanya remix ya wimbo wa “Wapo” kwa kuongeza maneno niliyoshauriwa na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine kutoka kwa wananchi pia niko tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi,” alisema Ney wa Mitego.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii nchini kutovuka mipaka katika utengenezaji wa kazi zao mpaka kufikia hatua ya kuvunja Sheria na taratibu za nchi.

Amesema kuwa  wasanii ni nguzo muhimu katika nchi sio kwa kufanya kazi ya  kuburudisha na kuelimisha bali katika kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana kwa malezi na makuzi ya wanajamii.

“Niwaombe wasanii nchini kuzingatia Sheria na taratibu za nchi katika utunzi wao na utenegenezaji wao wa kazi zao,” alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Aidha ameongeza kuwa Serikali haina nia ya kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue kuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu wote.

Share:

Leave a reply