Neymar atajwa kuwa mchezaji ghali zaidi duniani

1032
0
Share:

Staa wa soka anayekipiga wa Barcelona, Neymar ametajwa kuwa mchezaji ni ghali zaidi duniani akiwapita mastaa wengine ambao wanatajwa kuwa wakubwa zaidi yake akiwepo mchezaji mwenzake wa Barcelona, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia 2016.

Jambo hilo la Neymar kuwa mchezaji ghali duniani limejulikana kupitia utafiti ambao umefanywa na kampuni ya tafiti za soka ya CIES Football Observatory ambayo imesema kwasasa Neymar ana thamani ya Euro milioni 246.8.

Katika utafiti huo, Lionel Messi ameshika nafasi ya pili akiwa na thamani ya Euro milioni 170.5 na Paul Pogba akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na thamani ya Euro milioni 155.3 huku Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya saba kwa kuwa na thamani ya Euro Milioni 126.

Aidha CIES walisema vigezo walivyotumia kuchagua wachezaji hao ni uwezo wa mchezaji uwanjani, msaada anaotoa kwa timu yake, magoli anayofunga na dakika anzocheza pia kuangalia umri na mkataba alionao katika klabu anayoichezea.

Share:

Leave a reply