Neyo atua jijini Dar es Salaam usiku huu

290
0
Share:

Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Dar es Salaam usiku huu tayari kutumbuiza katika tamasha kubwa la Jembeka Festival 2016 litakalofanyika jijini Mwanza siku ya Jumamosi Mei 21 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa nchini Diamond Platnumz atapanda katika jukwaa hilo sambamba na wasanii wengine wa hapa nchini watakaosindikiza tamasha hilo.

Tamasha la Jembeka Festival 2016 limeandaliwa kwa udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM.

#JembekaNaVodacom

#JembekaNaCocacola

#JembekaFestival2016

#ILoveRockCityMwanza.

#ILoveRockCityMwanza.

Neyo Landed at Julius Nyerere International Airport

Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani Neyo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu akiwa amefuatana na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (tisheti nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Tamasha la Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (tisheti nyeupe).

Neyo in Dar es Salaam, Tanzania

Msanii kutoka nchini Marekani Neyo akielekea kwenye usafiri maalum alioandaliwa.

Sebastian Ndege

Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe FM ya jijini Mwanza ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Jembeka Festival 2016, Dr. Sebastian Ndege akiongozana na mmoja wa wageni walioambatana na msanii Neyo mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Neyo at Hyatt Regency - The Kilimanjaro

Mwanamuziki Neyo akiwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro na kupokelewa na Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay (mwenye suti nyeusi).

TagsNeyo
Share:

Leave a reply