NHC yapanga kurudia tena zoezi la kuwaondoa wadaiwa sugu

412
0
Share:

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutoa taarifa ya madeni ya idara na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na watu binafsi, imesema itawachukulia hatua wadaiwa sugu wasiopunguza madeni yao hadi sasa.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa NHC, Raymond Mndolwa amewahimiza wadaiwa hao kuanza kulipa madeni yao kabla ya mwaka huu kuisha.

“Pamoja na watu binafsi kulipa, wapo baadhi wameendelea kulimbikiza madeni. Tunawataarifu wapangaji binafsi wa makazi na biashara kwamba zoezi la kuwaondoa wanaodaiwa wote limeanza,” amesema.

Mndolwa ametaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kwa wadaiwa sugu kuwa ni kuondolewa kwenye majengo ya shirika na kuuza samani zao kufidia deni linalodaiwa, kuwatoa wadaiwa hao kwenye vyombo vya habari, kuwapeleka mahakamani ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Tunawahimiza wapangaji wetu kutimiza wajibu wao ili kuepuka usumbufu hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka,” amesema.

Share:

Leave a reply