NHIF wataka maoni kutoka kwa wanachama wastaafu

260
0
Share:
NHIF

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewataka wanachama wastaafu wanaohudumiwa na mfuko huo kutoa maoni na ushauri wa namna ya kuboresha huduma zitolewazo kwa ajili yao.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Bw.Eugin Mikongoti alipokua akiongea na wanachama wastaafu katika mkutano ulioandaliwa na NHIF.

“Hatukuwahi kuwa na mkutano maalumu wa wanachama wastaafu,ndiyo maana mkutano huu kwetu ni wa kihistoria na tunaamini ni muhimu kukutana na wastaafu peke yao ili kutoka kwao tusikie, siyo tu huduma nzuri wanazozipata bali pia changamoto wanazozikabili ili kwa pamoja tuweke mkakati wa kuzitatua”alisema Mikongoti.

Bw. Mikongoti ameongeza kuwa, wakati wote wamekua wakipokea na kuzingatia ushauri na maoni ya wadau wake wote, kwahiyo wanatarajia mkutano huu na wanachama wastaafu utakua ni uwanja mzuri wa kubadilishana mawazo na kupata ushauri wa namna ya kuboresha zaidi huduma zao.

Eugin Mikongoti

Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Bw.Eugin Mikongoti akiongea na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wanachama wastaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Aidha,Mwenyekiti wa kikao cha wastaafu,George Yambesi amewasihi wastaafu wenzie wafuatilie kwa makini na waulize maswali kwa kadiri watakavyoweza ili wawe na uelewa mpana kuhusu huduma za mfuko wa NHIF kwakua hii ndio fursa yao maana  hawapo kwenye ajira na hivyo sio rahisi kupata taarifa za mara kwa mara.

Pia Bw. Yambesi kwa niaba ya wenzake ameipongeza Serikali  kwa kuufanya Mfuko huu kutoa huduma za matibabu kwa wastaafu pia amewashukuru viongozi waasisi wa Mfuko kwa kuweka misingi bora ya kuwashughulikia wastaafu bila kukata tamaa.

Naye mmoja wa wastaafu kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa Ngalinecha Ngahyoma anaishukuru NHIF kwa kuwasaidia wastaafu kupata matibabu maana gharama za matibabu ni kubwa bila kuwa na bima za afya wastaafu wasingeweza kulipia huduma hizo.

Imeandaliwa na Jacquiline Mrisho -MAELEZO

Emmanuel Humba

Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

George Yambesi

Mwenyekiti wa kikao cha wanachama wastaafu Bw.George Yambesi akisikiliza jambo kwa umakini kutoka kwa mmoja ya wastaafu (hayupo pichani).

01

Baadhi ya wanachama wastaafu walioshiriki katika kikao kilichoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

NHIF

Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakijitambulisha mbele ya wanachama wastaafu (Hawapo pichani).

Share:

Leave a reply