Nmb Bank kutumia maonesho ya Saba Saba kutoa elimu kuhusu akaunti ya FANIKIWA

371
0
Share:

Bank ya NMB Tanzania imesema kuwa itatumia siku 11 za maonesho ya Saba Saba ambayo yalianza Juni, 28kutoa elimu kwa wananchi kuhusu akaunti mpya ambayo imeanzishwa na benki hiyo ya Fanikiwa.

Katika taarifa ambayo imetolewa na benki hiyo imesema akaunti hiyo ni nzuri kwa wananchi hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati kwani itawawezesha wafanyabiashara wadogo kupata huduma bora kutoka NMB.

“Sisi kama benki tumejiandaa kutoa huduma mbali mbali za kifedha kwa wateja wetu ili kukidhi watakwa yao pamoja na kutoa elimu juu ya bidhaa na huduma zetu kama isemavyo   kauli mbiu ya maonyesho haya ‘Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda’,

“Tunalenga kutumia fursa hii kuelimasha umma kuhusu Akaunti yetu mpya ya FANIKIWAmahususi kwa ajili ya wafanya biashara wadogo wadogo wakiwemo mama lishe, wakaanga chips, wauza magenge n.k,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa akaunti ya Fanikiwa itamwezesha mfanyabishara kutambulika kama mteja mfanyabiashara na atakuwa mwanachama kweye klabu za biashara za NMB (NMB Business Club) ambayo itamwezesha kupata mkopo mpaka milioni 30.

Pia huduma zingine za NMB zitakuwa zikitolewa ikiwepo akaunti maalum kwa ajili ya watoto iitwayo Wajibu ambayo inahusisha Mtoto akaunti, Chipukizi akaunti na Mwanachuo akaunti pia kutoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa kumfungulia mtoto akaunti na kumjengea tabia ya kuweka akiba kwa ajili ya baadaae.

Pamoja na hayo pia katika banda la NMB kutatolewa elimu kuhusu NMB Wakala na kwa watu ambao watakuwa wanahitaji kuwa mawakala watasajiliwa ili kutoa huduma kwa wateja wa NMB ambao wanataka kutoa pesa au kuweka pesa kupitia mawakala ambao wapo maeneo mbalimbali nchini.

Share:

Leave a reply