NMB Bank yazindua kituo cha biashara Kahama

617
0
Share:
Benki ya NMB Tanzania imezindua rasmi kituo cha biashara mjini Kahama (Kahama Business Centre) ambacho kitakuwa kikitoa huduma kwa wananchi wa kanda ya ziwa ikijumuisha mikoa mitatu ya Shinyanga, Tabora na Kigoma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema kituo hicho ni sehemu ya mpango wa NMB kuwasogezea wananchi huduma bora mahsusi kwa wajasiriamali ambapo pamoja na kufungua kituo hicho pia itatoa mafunzo kwa wajasiriamali.

“Hili tawi ambalo tumezindua leo ni sehemu ya mpango wetu wa kuwasaidia wajasiriamali, muda umefika tunahitaji uhusiano mkubwa baina yetu na wateja wetu ambao ni wajasiriamali,” alisema Bussemaker.


Kituo cha Kahama kinakuwa kituo cha 10 ambapo lengo kubwa ni kutoa huduma kwa karibu kwa wajasiriamali kuanzia wadogo hadi wakubwa na maeneo mengine ambayo kuna vituo kama hivyo ni Dodoma, Kariakoo, Sinza, Arusha, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara na Mwanza.

Share:

Leave a reply