NMB yaikabidhi MSD milioni 25 kusaidia duka la dawa kwa jamii

209
0
Share:
Benki ya NMB imekabidhi kiasi cha sh. Milioni 25 kusaidia Bohari Kuu ya Dawa (Medical Stores Department) katika kuboresha uendeshaji wa maduka na uendelezaji wa ujenzi wa maduka katika mikoa tofauti. Hundi hiyo ilikabidhiwa katika ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa wateja wakubwa wa NMB Richard Makungwa, alisema msaasa huo ni muendelezo wa mahusiano yao na Bohari ya Dawa (MSD). 
 
Ujenzi wa bohari hiyo ya dawa itasaidia kupunguza adha ya upatikanaji wa dawa hasa kwa wananchi wa Rukwa kwani kulikuwa na umbali mkubwa kufikia huduma hiyo. Sekta ya afya ni moja kati ya kipaumbele kikubwa sana kwa benki ya NMB ikiwa ni njia ya mojawapo ya kujali jamii inayotuzunguka. Naye Mkurugenzi Mkuu wa (MSD) Laurean Bwanakunu ameishukuru benki ya NMB kwa kuwa karibu nao hasa katika suala zima la kusaidia maendeleo ya jamii. 
 
Mpaka sasa kuna vituo saba ambavyo ni pamoja na kilichopo nje ya Hospitali ya Taifa (MNH), Sekoture Mwanza, Mount Meru Arusha, nje ya Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Katavi, Ruangwa iliyopo mkoa wa Lindi na Chato Geita.
Share:

Leave a reply