NMB yazindua huduma ya kuwasaidia wananchi kumiliki nyumba

508
0
Share:

Beki ya NMB imezindua huduma mpya inayoitwa NMB Mortgage ambayo itawapa nafasi wananchi ambao ni wateja wa benki hiyo na ambao sio wateja kupata mkopo ambao utawawezesha kumiliki nyumba na kwa mtu ambaye atatumia huduma hiyo kati ya Novemba 1, 2017 hadi Machi 31, 2018 hakutakuwa na gharama za uendeshaji.

Akizindua huduma hiyo Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Mauzo ya Benki ya NMB, Omari Mtiga alisema huduma hiyo mpya itakuwa na vipengele vitatu na itampa nafasi kila mwananchi kuomba hata kama sio mteja wa benki ya NMB.

 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Mauzo ya Benki ya NMB, Omari Mtiga akizungumza kuhusu huduma ya NMB Mortgage.

Alisema mkopo utakaotolewa utahusisha ujenzi wa nyumba pekee na mkopo wa fedha utakaotolewa utaanzia milioni 10 hadi milioni 700 na mkopo utalipwa ndani ya muda wa miaka 15 tangu uchukuliwe lakini ukimpa nafasi mkopaji kama akiweza kulipa hata kwa muda mfupi.

“Tunafahamu kuwa mwanadamu ana mambo ya muhimu na moja ya jambo hilo ni lazima awe na makazi ya kuishi, NMB kwa kuwajali wananchi tumewaletea huduma ya NMB Mortgage ambayo tutakuwa tukiwasaidia wananchi kutimiza ndoto zao za kumiliki nyumba kwa kuwapa mkopo,

“Huduma hii ina mikopo ya aina tatu, kuna mkopo wa kuanza kujenga nyumba yote, kuna mkopo wa kama nyumba imefika kwenye renta unaweza kuchukua mkopo wa kuezeka na kusafisha nyumba ndani na kuna mkopo kama unataka kuifanyia nyuma marekebisho.” alisema Mtiga.

Naye Mkuu wa huduma ya NMB Mortgage, Miranda Lutege alisema wananchi wanaoweza kupata huduma hiyo ni pamoja na wafanyakazi, watu waliojiajiri, mfanyabiashara na hata mtu ambaye ni Mtanzania lakini anaishi nje ya Tanzania na anataka kujenga nyumba hapa nchini.

Mkuu wa huduma ya NMB Mortgage, Miranda Lutege akizungumza jinsi ambayo wananchi wanaweza kupata huduma hiyo ambayo wateja wa benki zote nchini wataipata.

Lutege alisema kwa mwananchi ambaye anapenda kuchukua mkopo kutoka NMB Mortgage anaweza kutembelea tawi lolote la NMB nchini na atachukua fomu ambayo ataijaza na kutuma maombi ambapo ili mtu apate mkopo anatakiwa kuambatanisha baadhi ya vitu ambavyo vitathibitisha kweli pesa ambayo anaiomba itatumika katika kujenga au kuifanyia matengenezo nyumba.

Share:

Leave a reply