Nwanko Kanu awafariji wagonjwa wa moyo wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

318
0
Share:

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles Nwankwo Kanu leo ametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hopsitali ya Taifa Muhimbili (NH) kwa lengo la kuwajulia
hali wagonjwa wa moyo ambao wamelazwa katikaTaasisi hiyo, pia kubadilishana
uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi hiyo.

Akizungumza  baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuwapa pole.

Katika mazungumzo yake pamoja na mambo mengine Kanu ameonyesha nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi ya Moyo ili kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.

Pia, ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona.

Kwaupande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Godwin Godfrey amesema tangu Julai mwakaja na mpaka sasa taaissi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.

Nwankwo Kanu alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo aliamua
kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa The Kanu Heart Foundation. 

Kanu amechezea timu ya Taifa ya Nigeria yaSuper Eagles, Arsenal, Inter Milan, West Bromwich Albion, Portsmouth na AFC Ajax. Amenyakua tuzo nyingi kutokana na umairi wake soka.

Habari na picha zote  kwa hisani ya John Stephen, Ofisa Uhusiano  wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH)

7392a281-73dd-49f2-8f08-8743de919325Fatuma Shaban akipokeazawadi kutoka kwa Nwankwo Kanu kwa niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.

03d13fb2-5e2f-408c-8a9a-377f144c9c2cMchezaji huyo akiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) leo.

186344b5-39b3-46a3-af63-3a8de982eff3 Mgonjwa Mariam Omary akifurahia jambo baada ya mchezaji huyo kumjulia hali leo
kwenye taasisi hiyo.

Share:

Leave a reply